• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 23, 2016

  KIBADENI HAELEWI MUSTAKABALI WAKE JKT RUVU

  Na Somoe Ng'itu, DAR ES SALAAM
  KOCHA mkongwe nchini, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden' amesema bado hajasaini mktaba wa kuendelea kuifundisha timu ya JKT Ruvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
  Kibadeni aliisaidia JKT Ruvu kubaki kwenye Ligi Kuu baada ya kuchukua nafasi ya Freddy Felix Minziro, huku timu tatu za Tanga, JKT Mgambo, Coastal Union na African Sports zikishuka daraja.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana, Kibadeni alisema kuwa endapo atabaki kwenye kikosi hicho, timu hiyo haitapambana kubaki Ligi Kuu, badala yake itakuwa inawania ubingwa wa Bara.
  Alisema kuwa katika kuhakikisha JKT Ruvu inakuwa moja ya timu tishio, amependekeza ifanye usajili wa wachezaji wapya sita ambao wataongeza nguvu na kutoa ushindani katika kila mchezo watakaoshuka dimbani kusaka pointi.
  "Nimewaachia wenyewe, kama wanaona ninafaa sawa, ila endapo nitakuwa na hiyo timu msimu ujao, ninawahakikishia itakuwa tofauti, si ile inayopambana kubaki ligi kuu, sasa itashindana na wale wanaosaka ubingwa," aliongeza Kibadeni.
  Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba alisema kuwa soka la Tanzania analijua, hivyo anafahamu mbinu za kukiimarisha kikosi hicho kuanzia mwanzo wa msimu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIBADENI HAELEWI MUSTAKABALI WAKE JKT RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top