• HABARI MPYA

  Wednesday, June 22, 2016

  STRAIKA WA GHANA APANIA KUIFUNGIA MABAO ZAIDI AL AHLY

  MSHAMBULIAJI wa Ghana, John Antwi (pichani kulia) amesema anapaswa kuongeza bidii ili kuisaidia klabu yake baada ya kuanza vibaya mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa 3-2 na Zesco United ya Zambia.
  Katika mchezo huo wa ufunguzi wa hatua ya makundi, Antwi alifunga mabao yote mawili Ahly dhidi ya matatu ya Zesco. Na nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyejiunga na Ahly kabla ya msimu huu kutoka Al Shabab Riyadh ya Saudi Arabia amesema lazima apambane kuisaidia timu yake katika mashindano hayo.
  “Tulikuwa tuna mchezo mzuri japokuwa tulifungwa, timu ya Zesco ilikuwa ina nguvu sana,” alisema na kuongeza; “Nimefunga mabao mawili na kwangu ilitokana na juhudi za pamoja hivyo naheshimu mchango wa wachezaji wenzangu. Sasa natakiwa kujituma zaidi na kufunga mabao zaidi ili kuisaidia timu yangu," alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STRAIKA WA GHANA APANIA KUIFUNGIA MABAO ZAIDI AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top