• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 25, 2016

  MAGULI AIPIGA CHINI SUPER SPORT NA KUTIMKIA OMAN

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Elias Maguli ameondoka mapema wiki hii kwenda Oman kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa wakati pia alikuwa ana mwaliko wa kwenda kujaribiwa SuperSport United ya Afrika Kusini.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo, Wakala aliyekuwa anashughulikia mpango wa Maguli kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini, Rodgers Mathaba amesema kwamba amesikitishwa sana na kitendo kilichofanywa na mchezaji huyo.
  “Mimi nimehangaika sana kumpatia nafasi huku, imepatikana nataka kumtumia tiketi napewa taarifa amekwenda Afrika Kusini. Imenisikitisha sana,”amesema.
  Elias Maguli wakati anaondoka Dar es Salaam mapema wiki hii kwenda Oman
  Rodgers amesema kwamba Maguli alikuwa ana nafasi kubwa ya kusajiliwa na SuperSport baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kupitia video ya baadhi ya mechi alizocheza ikiwemo dhidi ya Kenya mjini Nairobi mwezi uliopita ambako aloifunga bao katika sare ya 1-1 na kuridhishwa naye.
  “Kwa upande wangu, nilicheza nafasi yangu vizuri, Maguli alikuwa anakuja hapa kuwathibitishia tu na kusaini dili zuri, lakini amekwenda Oman, si vibaya, ni chaguo lake, ila wachezaji wa Tanzania hawajui wanachokitaka,”amesema kwa masikitiko Mathaba.
  Raia huyo wa Afrika Kusini ambaye Mei mwaka huu aliwaalika pia kwa majaribio Watanzania wengine, kiungo Omar Wayne na mshambuliaji Ibrahim Hajib alisema kwamba kwa sasa hajisikii tena kufanya kazi na Watanzania baada ya kitendo cha Maguli.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAGULI AIPIGA CHINI SUPER SPORT NA KUTIMKIA OMAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top