• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 24, 2016

  'MIDO' MKENYA VICTOR WANYAMA ATUA SPURS KWA PAUNI MILIONI 11

  KLABU ya Tottenham Hotspur imetangaza kumsajili kiungo Mkenya, Victor Wanyama kwa dau la Pauni Milioni 11 kutoka Southampton, zote za England.
  Nyota huyo wa Harambee Stars, sasa anaungana tena na kocha wake wa zamani, Mauricio Pochettino.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, aliyekaribia kujiunga na Spurs msimu uliopita, lakini akalazimishwa kubaki Uwanja wa St Mary's Stadium, amesaini Mkataba wa miaka mitano kuhamia Uwanja wa White Hart Lane.
  Wanyama alisajiliwa kutoka Celtic Julai mwaka 2013, lakini amekataa ofa ya kuongeza Mkataba Southampton na angeweza kuondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu ujao.
  Kiungo wa Kenya, Victor Wanyama akiwa ameshuka skafu ya Spurs baada ya kukamilisha uhamisho wake leo  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  WASIFU WA VICTOR WANYAMA CAREER

  2008-2011: Beerschot
  2011-2013: Celtic
  Tangu 2013: Southampton 
  Kiungo huyo wa ulinzi, ameandika kwenye tovuti yake kuwashukuru mashabiki wa Southampton. Amesema: 'Nakuandikia kwa moyo mzito kukutangazia kwamba nitaondoka Southampton FC. 
  "Kama ambavyo unaweza kuona ni kwa hisia kali ninaweza kukuambia kwaheri kuaga katika klabu ambayo imenipa nafasi ya kuwa Mkenya wa kwanza kucheza katika Ligi Kuu ya England,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'MIDO' MKENYA VICTOR WANYAMA ATUA SPURS KWA PAUNI MILIONI 11 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top