• HABARI MPYA

  Tuesday, June 28, 2016

  PLUIJM AMUANZISHA DOGO MAHADHI, CHIRWA YANGA NA MAZEMBE, JUMA ABDUL AREJEA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Juma Mahadhi atacheza mechi yake ya kwanza Yanga leo, baada ya kupangwa katika mchezo dhidi ya TP Mazembe.
  Yanga inawakaribisha TP Mazembe ya DRC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
  Na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amepanga wachezaji wapya wawili aliowasajili katika dirisha dogo la usajili wa Shirikisho la Soka Afrika Afrika (CAF).
  Juma Mahadhi anaanza leo Yanga na TP Mazembe
  Mbali na Mahadhi aliyesajiliwa kutoka Coastal Union ya Tanga iliyoteremka daraja, Pluijm pia amempanga kiungo Obrey Chirwa kutoka Zambia, aliyesajiliwa kutoka FC Platinums ya Zimbabwe.
  Kipa Deo Munishi ‘Dida’ ataendelea kusimama langoni, beki Juma Abdul aliyekosa mchezo uliopita dhidi ya Mo Bejaia anarudi leo beki ya kulia, wakati Mbuyu Twite atacheza beki ya kushoto.
  Mabeki wa kati watakuwa ni Kevin Yondan na Mtogo mwenye asili ya Ivory Coast, Vincent Bossou wakati kiungo wa ulinzi ni Mzimbabwe Thabani Kamusoko.
  Viungo wengine ni Mahadhi, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke wakati washambuliaji ni Chirwa na Donald Ngoma.   
  Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Donald Ngoma.
  Katika benchi wapo; Ally Mustafa ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Andrew Vincent ‘Dante’, Pato Ngonyani, Said Juma ‘Makapu’, Matheo Anthony na Geoffrey Mwashiuya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AMUANZISHA DOGO MAHADHI, CHIRWA YANGA NA MAZEMBE, JUMA ABDUL AREJEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top