• HABARI MPYA

  Monday, June 27, 2016

  MESSI ASTAAFU KUICHEZEA ARGENTINA KWA KILIO NA MACHOZI

  MAUMIVU ya moyo yamemshinikiza Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina baada ya jana kufungwa katika fainali ya tatu mfululizo ya Copa America ndani ya miaka mitatu.
  Messi si mgonjwa wa moyo, bali ameumizwa n a kitendo cha kukosa penalti ya kwanza Argentina ikifungwa kwa penalti 4-2 katika fainali ya Copa America Centenario baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 120.
  Lionel Messi amestaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina 

  Messi ambaye alimwaga machozi na kilio baada ya mechi hiyo alizungumza na Televisheni ya Argentina baada ya mechi na kufafanua uamuzi wake. "Ni hivyo. Mimi baso na timu ya taifa,"alisema. 
  "Si kwangu. Hii ni fainali ya nne. Uamuzi umefanyika, nafikiri hivyo. [kushinda] ndicho ninachoitaka zaidi. Sikuja. nafikiri ni hivyo. Hivyo ndivyo ninavyojisikia kwa sasa, ninachofikiria. ni maumivu makubwa,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI ASTAAFU KUICHEZEA ARGENTINA KWA KILIO NA MACHOZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top