• HABARI MPYA

  Friday, June 24, 2016

  JOHN OBI MIKEL AITWA NIGERIA KIKOSI CHA OLIMPIKI YA BRAZIL 2016

  KOCHA wa timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya umri wa miaka ya 23, Samson Siasia amemuita Nahodha wa Super Eagles, John Mikel Obi (pichani kushoto) katika kikosi cha awali cha wachezaji 34 kwa kambi ya kujiandaa na michezo ya Olimpiki nchini Marekani.
  Kikosi hicho kitapunguzwa na kubaki na wachezaji 18 ambacho kitasafiri kwenda mjini Rio de Janeiro, Brazil baadaye mwaka huu kwenye michezo hiyo.
  Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) limesema kikosi cha Olimpiki kitaondoka wiki ijayo kwenda kwenye kambi ya maandalizi Marekani. 
  NFF imethibitisha kutakuwa na mchezo wa kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya Mexico nchini Mexico Jumamosi ya Julai 2, mwaka huu Uwanja wa Aguascalientes, ambao unamilikiwa na klabu ya Necaxa FC iliyopanda Ligi Kuu ya nchi hiyo.
  NFF imesema baada ya mchezo huo, U23 ya Nigeria itaendelea na kambi yake nchini Marekani na itacheza na Charleston Battery FC mjini Atlanta Jumamosi ya Julai 16, wakati pia kuna mpango wa kucheza na U23 ya Honduras Julai 27.
  Kikosi kamili cha awali cha Nigeria kwa ajili ya Olimpiki kinaundwa na Daniel Akpeyi (Chippa FC, Afrika Kusini), Yusuf Bala (Kano Pillars), Emmanuel Daniel (Enugu Rangers), Taiwo Abdulrahman (Kwara United), Ndubuisi Agu (FC Porto, Ureno), Junior Ajayi (CS Sfaxien, Tunisia), Stanley Amuzie (Olhanense FC, Ureno), Taiwo Awoniyi (Frankfurt FC, Ujerumani), Okechukwu Azubuike (Yeni Malatyaspor, Uturuki), Etor Daniel (Enyimba FC), Augustine Dimgba (Sunshine Stars), William Ekong (Haugesund FC, Norway), Saturday Erimuya (Kayseri Erciyespor, Uturuki), Oghenekaro Etebo (CD Feirense FC, Ureno), Imoh Ezekiel (Anderlecht, Belgium), Saviour Godwin (Ostende, Ubelgiji), Odion Ighalo (Watford FC, England), Kelechi Iheanacho (Manchester City, England), Alex Iwobi (Arsenal FC, England), Emiloju Julius (MFM FC), Kingsley Madu (AS Trencin, Slovakia), John Mikel Obi (Chelsea FC, England), Musa Muhammed (Istanbul Basaksehir, Uturuki), Usman Muhammed (CF Uniao, Ureno), Wilfred Ndidi (KRC Genk, Ubelgiji), Erhun Obanor (MFM FC), Godfrey Oboabona (Caykur Rizespor, Uturuki), Kenneth Omeruo (Chelsea FC, England), Sodiq Saliu (Seraing FC, Ubelgiji), Abdullahi Shehu (CF Uniao, Ureno), Moses Simon (KAA Gent, Ubelgiji), Seth Sincere (Rhapsody FC), Ndifreke Udo (Abia Warriors), Aminu Umar (Osmalispor, Uturuki) na Sadiq Umar (AS Roma, Italia)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOHN OBI MIKEL AITWA NIGERIA KIKOSI CHA OLIMPIKI YA BRAZIL 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top