• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 26, 2016

  BAFANA BAFANA WATWAA TAJI LA NNE LA COSAFA

  TIMU ya taifa ya Afrika Kusini imetwaa taji la nne la Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika, COSAFA Castle baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Botswana katika fainali ya mwaka 2016 jana Uwanja wa Sam Nujoma mjini Windhoek, Namibia.
  Shukrani kwao, Gift Motupa aliyefunga mabao mawili kwa penalti na Thabiso Kutumela aliyefunga lingine.
  Bafana Bafana iliyo chini ya kocha mzalendo, Shakes Mashaba sasa inazifikia Zambia na Zimbabwe zilizotwaa taji hilo mara pia kila moja.

  Viongozi na wachezaji wa Afrika Kusini wakifuarahia jana baada ya fainali Uwanja wa Sam Nujoma mjini Windhoek, Namibia

  Haikuwa bahati yao Botswana, kwani walicheza soka ya kuvutia katika mashindano ya mwaka huu na hata katika mchezo wa jana walitangulia kwa mabao Onkabetse Makgantai na Kabelo Seakanyeng.
  Katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu, Swaziland iliifunga 1-0 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), bao pekee la Ndzinisa dakika ya 41.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BAFANA BAFANA WATWAA TAJI LA NNE LA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top