• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 23, 2016

  VARDY AKUBALI KUONGEZA MKATABA MPYA LEICESTER CITY

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Jamie Vardy amekubali kusaini Mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuchezea klabu yake, Leicester City na kukataa ofa ya kujiunga na Arsenal.
  Mustakabali wa mkali huyo wa mabao wa England umekuwa haueleweki tangu Arsene Wenger atangaze ofa ya Pauni Milioni 20 kumnunua Juni 3, mwaka huu, lakini ameipiga chini ofa hiyo na kuamua kubaki Uwanja wa King Power.
  Baada ya Arsenal kumpa ya mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki, Leicester City nayo imemuongezea mshahara mchezaji huyo hadi pauni 100,000 kwa wiki na Vardy atasaini Mkataba mpya atakaporejea kutoka kwenye Euro 2016 nchini Ufaransa.

  Vardy aliisaidia Leicester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England akifunga jumla ya mabao 24 msimu uliopita


  TAKWIMU ZA MSIMU ULIOPITA ZA JAMIE VARDY LEICESTER 

  Mechi alizocheza: 38
  Mabao aliyofunga: 24
  Pasi za mabao alizotoa: 8
  Dakika alizocheza: 3,210
  Dakika kwa bao: 134
  Mbali ya mshahara mkubwa zaidi, lakini Vardy angenufaika zaidi kwa kipato Uwanja wa Emirates kutokana na hali nzuri ya kiuchumi na sera za malipo za Arsenal ukilinganisha na Leicester.
  Iwapo atasaini Mkataba mpya, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atadumu King Power hadi mwaka 2020 atakapofikisha umri wa miaka 33 – jambo ambalo ni habari njema kwa kila mmoja ndani ya Leicester City.
  Vardy alikuwa chachu ya mafanikio ya Leicester City msimu uliopita ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, akifunga jumla ya mabao 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VARDY AKUBALI KUONGEZA MKATABA MPYA LEICESTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top