• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 27, 2016

  KAMISAA ATAKA WATU 40,000 TU UWANJANI KESHO YANGA NA TP MAZEMBE

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam una uwezo wa kuchukua watu 60,000, lakini kesho utafungwa wakati wa mchezo wa Yanga na TP Mazembe ya DRC baada ya mashabiki 40,000 kuingia.
  Hayo ni maagizo ya Kamisa wa mchezo huo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, ambao mashabiki wataingia bure, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda.
  Na hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alipozungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
  Muro amesema kwamba mashabiki watakaobahatika kuingia uwanjani ni wale ambao watafika mapema na kwamba Yanga itatekeleza agizo la Kamisaa la kufunga mageti yote wakitimia watu 40,000.
  Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' (kulia) akiwaongoza wachezaji wenzake katika mchezo na Sagrada Esperanca ya Angola
  Muro amesema kwamba kutakuwa na ulinzi mkali wa askari Polisi kesho kuhakikisha kwamba hazitokei vurugu za aina yoyote na watu wanaangalia mchezo na kurejea nyumbani salama.
  Wapinzani, Mazembe waliwasili usiku wa jana na mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu alipata mapokezi mazuri baada ya kutokeza nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). 
  Mazembe imekuja na kikosi cha wachezaji 18 ambao ni; Robert Kidiaba, Sylvain Gbohou, Issama Mpeko, Joel Kimwaki, Thomas Ulimwengu, Christian Koume,
  Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope,
  Jose Badibake, Kissi Boateng, Roger Assale, Rainford Kalaba, Deo Kanda, Adama Traore, Chriastian Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.
  Maofisa wa benchi la Ufundi waliokuja ni Theobald Binamungu, Mohamed Kamwanya,
  Dony Kabongo, Frederic Kitengie na Andre Ntime.
  Madaktari ni Hurbert Velud, Pamphile Mihayo, Mhudumu Richard Mubemb na Maofisa wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Heritier Yinduka, Arther Kikuni na Meshack Kayembe.
  Katika mechi za kwanza za kundi hilo, Mazembe ilishinda 3-1 nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana wakati Yanga ilifungwa 1-0 ugenini na MO Bejaia ya Algeria Jumapili iliyopita.
  Waamuzi wa mchezo huo ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
  Yanga ilirejea nchini kwa awamu mbili Ijumaa na Jumamosi kutoka Antalya, Uturuki ilipokuwa imeweka kambi kujiandaa na mchezo huo mara tu baada ya mechi na MO Bejaia.
  Kikosi kamili cha Yanga kilichokuwa kambini mjini ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
  Mabeki; Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Vincent Bossou na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
  Viungo; Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya na Obrey Chirwa.
  Washambuliaji; Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe, chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAMISAA ATAKA WATU 40,000 TU UWANJANI KESHO YANGA NA TP MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top