Wachezaji wa England kutoka kushoto Dele Alli, Chris Smalling na Wayne Rooney wakiwa wanyonge baada ya kufungwa bao la pili wakilala 2-1 mbele ya Iceland katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Euro 2016 Uwanja wa Allianz Riviera mjini Nice, Ufaransa na kutolewa. England ilitangulia kwa bao la penalti la Nahodha Rooney dakika ya nne baada ya raheem Sterling kuangushwa kwenye boksi na kipa Hannes Halldorsson, kabla ya Ragnar Sigurdsson kuisawazishia Iceland dakika mbili baadaye na Kolbeinn Sigthorsson kufunga la pili dakika ya 18 na sasa watamenyana na wenyeji Ufaransa katika Robo Fainali, huku Three Lions wakiendeleza rekodi yao ya kutoshinda mechi ya mtoano tangu Euro 2006 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Watch: Lille midfielder Ethan Mbappe shown red card for ugly elbow
-
Ethan Mbappé was shown a red card in Lille's Champions League match against
Real Betis on Tuesday.
18 hours ago



.png)
0 comments:
Post a Comment