• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 26, 2016

  KAVUMBANGU: NIKO TAYARI KUJIUNGA NA TIMU YOYOTE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu amesema yuko tayari kusaini timu yoyote hata ya nje ya Dar es Salaam baada ya kumaliza Mkataba wake Azam FC.
  Azam FC imemua kuachana na Kavumbangu baada ya misimu miwili tangu ajiunge nao, akitokea kwa wapinzani, Yanga SC.
  Na Mrundi hiyo aliyefunga mabao 23 katika mechi 60 Azam FC, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana mjini Dar es Salaam kwamba yuko tayari kupokea ofa ya timu nyingine yoyote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Didier Kavumbangu amesema yuko tayari kusaini timu yoyote hata ya nje ya Dar es Salaam

  “Mimi nipo kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wangu Azam FC, na ninakaribisha timu yoyote kufanya mazungumzo name,”alisema.
  Alipoulizwa kuhusu mipango ya kujiunga na Mbeya City, Kavumbangu alisema kwamba alifanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo, lakini hawakufikia mwafaka.
  “Milango bado ipo wazi hata kwa wao Mbeya City, wakiweza kuongeza kidogo ofa yao, naweza kujiunga nao, mimi ni mchezaji naangalia maslahi,”alisema.
  Kavumbangu aliingia Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2012 akitokea Atletico ya kwao, Burundi na katika misimu miwili alicheza jumla ya 63 na kufunga mabao 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAVUMBANGU: NIKO TAYARI KUJIUNGA NA TIMU YOYOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top