• HABARI MPYA

  Monday, June 27, 2016

  NI CHILE TENA MABINGWA COPA AMERICA 2016, PENALTI YA MESSI YAPOTEZA MWELEKEO

  Kipa wa Chile, Claudio Bravo akiinua Kombe la Copa America Centenario baada ya kulitwaa usiku wa kuamkia leo kwa kuifunga Argentina kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 Uwanja wa MetLife, East Rutherford mjini New Jersey, Marekani. Mwanasoka bora wa dunia, Lionel Messi alikosa penalti ya kwanza ya Argentina sawa na Lucas Biglia aliyekosa ya nne. Waliofunga penalti za Argentina ni Javier Mascherano na Sergio Aguero wakati za Chile zilifungwa na N. Castillo, C. Aránguiz, J. BeausejourF. Silva huku  A. Vidal akikosa ya kwanza tena  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI CHILE TENA MABINGWA COPA AMERICA 2016, PENALTI YA MESSI YAPOTEZA MWELEKEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top