• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 28, 2016

  TSHABALALA: BADO NIPO NIPO SANA SIMBA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kushoto wa Simba SC, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amepuuzia uvumi kwamba anataka kuihama klabu hiyo akisema kwamba ana Mkataba wa mwaka mmoja na ataendelea kuwapo Simba.
  “Mimi ninashangaa sana, sijui maneno mengine yanatoka wapi, mimi ni mchezaji halalai wa Simba na nina Mkataba wa mwaka mmoja mzima bado,”amesema leo akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE mjini Dar es Salaam.
  Kauli hiyo ya Tshabalala inafuatia kuwapo uvumi kwamba amebakiza miezi sita katika Mkataba wake Simba na anataka kujiunga na ama na Azam au Yanga.
  Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kwamba bado yupo yupo sana Simba 

  “Hapa nilipo hata kufikiria kuzungumza na klabu nyingine siwezi, kwa sababu nina Mkataba wa mwaka mzima na Simba. Niseme tu kwa sasa mimi ni mchezaji wa Simba na nitaendelea kuitumikia Simba msimu ujao, wapenzi na mashabiki wa Simba wapuuze uvumi wowote kuhusu mimi kuondoka.
  Pamoja na hayo, Tshabalala amesema wakati Simba inatarajiwa kuanza mazoezi wiki ijayo, lakini yeye tayari amekwishaanza kufanya mazoezi binafasi kujiweka fiti.
  “Mimi nimekwishaanza mazoezi yangu binafsi kama mchezaji kujiweka fiti kabla ya kwenda kuanza mazoezi ya timu. Nina kama wiki mbili sasa ninafanya mazoezi ya ufukweni na gym,”alisema.
  Tshabalala alijiunga na Simba SC misimu miwili iliyopita kutoka Kagera Sugar ya Bukoba na tangu hapo amekuwa beki tegemeo na chaguo la kwanza upande wa kushoto. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TSHABALALA: BADO NIPO NIPO SANA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top