• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 25, 2016

  VIINGILIO YANGA NA TP MAZEMBE HIVI HAPA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imetaja viingilio viwili tu katika mchezo wake wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam mchana wa leo, Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema viingilio hivyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP.
  Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu mjini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo ambao utaanza Saa 10:00 jioni.
  Jerry Muro (kushoto) akizingumza na Waandishi wa Habari leo Jangwani. Kulia ni Meneja Masoko, Omar Kaaya

  Huo utakuwa mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
  Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa watatu kutoka nchi tatu tofauti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
  Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VIINGILIO YANGA NA TP MAZEMBE HIVI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top