• HABARI MPYA

  Tuesday, June 28, 2016

  KALABA NJE MAZEMBE DHIDI YA YANGA, ULIMWENGU ANAANZA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJi tegemeo wa TP Mazembe ya DRC, Ranford Kalaba hatacheza dhidi ya Yanga jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kuwa majeruhi.
  Kalaba hayumo kabisa katika orodha ya wanaoshiriki mchezo wa leo, jambo ambalo hakika ni pigo kwa Mazembe katika mchezo huu wa ugenini.
  Mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emanuel Ulimwengu ameanzishwa pamoja na Koffi Christian na Christian Luyindama katika safu ya ushambuliaji.
  Ranford Kalaba (kushoto) akiwa na kocha Mfaransa, Hubert Velud wa Mazembe muda huu Uwanja wa Taifa kabla ya mchezo na Yanga 
  Thomas Ulimwengu (katikati) akipasha muda huu na wachezaji wenzake wa Mazembe
  Wachezaji wa Yanga wakipasha muda huu kabla ya mechi
  Vikosi kamili vya leo ni Yanga; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Donald Ngoma.

  Katika benchi wapo; Ally Mustafa ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Andrew Vincent ‘Dante’, Pato Ngonyani, Said Juma ‘Makapu’, Matheo Anthony na Geoffrey Mwashiuya.
  TP Mazembe; Sylvain Gbohoud Guelassiognon, Jean Kasusula, Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Rodger Asale, Adama Traore, Merveille Bope, Nathan Sinkala, Koffi Christian, Christian Luyindama na Thomas Ulimwengu.
  Benchi; Robert Kidiaba Muteba. Joel Kimwaki, Deo Kanda, Jonathan Bolingi, Daniel Nii Adjei, Jose Bodibake Mpongo, Richard Kissi Boateng na Jonas Sakuwaha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KALABA NJE MAZEMBE DHIDI YA YANGA, ULIMWENGU ANAANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top