• HABARI MPYA

    Friday, June 24, 2016

    UGANDA YAPANGWA NA 'VIGOGO' KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018

    TIMU ya taifa ya Uganda, maarufu The Cranes imepangwa katika Kundi E pamoja na Ghana, Misri na Kongo katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
    Uganda ndiyo pekee ya Afrika Mashariki na Kati, ukanda ulio chini ya CECAFA iliyobaki katika mbio za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
    Kundi A lina timu za Tunisia, Libya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Guinea, Kundi B kuna  Zambia, Cameroon, Algeria na Nigeria, Kundi C kuna Gabon, Mali, Ivory Coast na Morocco, wakati Kundi linaundwa na Senegal, Afrika Kusini, Burkina Faso na Cape Verde.
    Mechi za kwanza za makundi zitachezwa Oktoba mwaka 2016 na mshindi wa kila kundi ndiye atakayefuzu kuiwakilisha Afrika kwenye fainali hizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA YAPANGWA NA 'VIGOGO' KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top