• HABARI MPYA

  Thursday, June 30, 2016

  AZAM FC KUMKOSA SERGE WAWA MECHI YA NGAO NA YANGA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kati wa Azam FC, Serge Wawa Pascal atakosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi Yanga Agosti na pia atakosa mechi za mwanzo za msimu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Wawa aliumia Aprili mwaka huu akiichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia na tangu hapo amekuwa nje ya Uwanja.
  Na Daktari wa Azam FC, Juma Kwimbe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba Wawa raia wa Ivory Coast anatakiwa nje kwa miezi miwili zaidi na ataanza mazoezi mepesi Septemba.
  Serge Wawa Pascal atakosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi Yanga Agosti

  Wawa pamoja na beki mwingine tegemeo wa Azam FC, Shomary Kapombe walipelekwa Afrika Kusini wiki iliyopita kufanyiwa vipimo baada ya wote kukosekana tangu Aprili kwa maumivu.
  Na baada ya vipimo hivyo, Kwimbe amesema kwamba Kapombe ameruhusiwa kuanza mazoezi mepesi Julai 18 chini ya uangalizi wa daktari wa mazoezi – maana yake anaweza kurudi uwanjani mapema msimu ujao. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUMKOSA SERGE WAWA MECHI YA NGAO NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top