• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 29, 2016

  MEDEAMA YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA MO BEJAIA NYUMBANI

  MEDEAMA FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na MO Bejaia ya Algeria katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Sekondi-Takoradi mjini Sekondi, Ghana.
  Matokeo hayo ya 0-0 yanaifanya MO Bejaia ifikishe pointi nne na kuendelea kukamata nafasi ya pili katika kundi hilo, nyuma ya TP Mazembe ya DRC yenye pointi sita, baada ya kila timu kucheza mechi mbili, moja nyumbani na nyingine ugenini.
  Medeama FC imepata pointi ya kwanza leo katika Kundi A
  Na baada ya kupata pointi yake ya kwanza ikitoka kufungwa 3-1 katika mchezo wake wa kwanza na Mazembe mjini Lubumbashi Juni 19, Medeama inapanda kwa nafasi moja hadi ya tatu, ikiiteremshia nafasi ya nne Yanga ya Tanzania.
  Yanga ni timu pekee iliyofungwa mechi zote katika kundi hili hadi sasa, baada ya kufungwa 1-0 mara mbili mfululizo, kwanza na MO Bejaia Juni 19 Algeria na jana kufungwa 1-0 pia Mazembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Julai 7 Yanga watakuwa wenyeji wa Medeama, wakati Mazembe itasafiri kuifuata MO Bejaia Algeria. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MEDEAMA YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA MO BEJAIA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top