Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
PAZIA la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara litafungwa Jumamosi ya Mei 9, mwaka huu kwa mechi saba kuchezwa viwanja tofauti.
Polisi Moro imekwishaipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu na kundeleza rekodi yake ya kupanda na kuteremka msimu huo huo, wakati Ruvu Shooting, Prisons, Ndanda FC, Mgambo Shooting na Stand United zitakuwa zinagombea nafasi moja ya kubaki Ligi Kuu.
Ndanda wanacheza na Yanga SC ambayo tayari imeweka kabatini Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, je watapata huruma ya Jangwani wasiteremke daraja?
Ndanda wenye pointi 28 wanacheza na Yanga SC, ambayo tayari imetwaa ubingwa, Mgambo Shooting yenye pointi 28 wanacheza na Azam FC ambayo tayari imejinyakulia nafasi ya pili.
Timu hizo mbili kama zitapata ‘huruma’ ya wapinzani wao, Yanga na Azam na kushinda, maana yake zitafikisha pointi 31 na kuepuka balaa la kushuka.
Stand United yenye pointi 28 itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting yenye pointi 29, zote zina hali mbaya, wakati Polisi Moro yenye pointi 25 itakuwa mgeni wa Mbeya City yenye pointi 31, na Prisons wenye pointi 28 watakuwa wageni wa Kagera Sugar yenye pointi 31.
MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
1 Yanga SC 25 17 4 4 52 17 35 55
2 Azam FC 25 13 9 3 36 18 18 48
3 Simba SC 25 12 8 5 36 18 18 44
4 Mtibwa 25 7 10 8 24 24 0 31
5 Mbeya City 25 7 10 8 21 22 -1 31
6 Kagera 25 8 7 10 22 26 -4 31
7 JKT Ruvu 25 8 7 10 19 23 -4 31
8 Coastal U 25 7 10 8 19 24 -5 31
9 Ruvu Shoot 25 7 8 10 16 28 -12 29
10 Prisons 25 5 13 7 18 22 -4 28
11 Ndanda 25 7 7 11 20 29 -9 28
12 Mgambo 25 8 4 13 18 28 -10 28
13 Stand Utd 25 7 7 11 22 34 -12 28
14 Polisi Moro 25 5 10 10 16 26 -10 25
14 Polisi Moro 25 5 10 10 16 26 -10 25
Timu za Ligi Kuu msimu ujao zitaongezeka kutoka 14 hadi 16 na msimu huu timu zitashuka timu mbili, huku tayari timu za kupanda ni Majimaji ya Songea, Mwadui ya Shinyanga, Toto Africans ya Mwanza na African Sports ya Tanga.
Timu ipi itaungana na Polisi Moro kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.



.png)
0 comments:
Post a Comment