Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC jana imefungwa kwa mara ya kwanza katika baada ya mechi nane za nyumbani.
Yanga SC imefungwa mabao 2-1 jana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, umewafanya Azam FC wakate tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufikisha pointi 48, ambazo haziwezi kufikiwa na Simba SC waliokuwa wanaiwania pia nafasi hiyo.
Yanga SC waliingia kwenye mechi ya jana wakiwa tayari mabingwa baada ya kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.
Kabla ya jana, katika Ligi Kuu Yanga walifungwa mara ya mwisho na mahasimu wa jadi, Simba SC Machi 8, mwaka huu 1-0, bao pekee la Emmanuel Okwi.
Kutoka hapo, Yanga SC ilizifunga 2-1 Kagera Sugar, 2-0 Mgambo JKT, 3-1 JKT Ruvu, 8-0 Coastal Union, 3-1 Mbeya City, 3-2 Stand United, 5-0 Ruvu Shooting na 4-1 Polisi Moro.
Pazia la Ligi Kuu linatarajiwa kufungwa mwishoni mwa wiki, Jumamosi kwa mechi saba kupogwa viwanja tofauti; JKT Ruvu Vs Simba SC, Mtibwa Sugar Vs Coastal Union, Stand United Vs Ruvu Shooting, Mbeya City Vs Polisi Moro, Kagera Sugar Vs Prisons, Ndanda FC Vs Yanga SC na Azam FC Vs Mgambo JKT.

![]() |
| Brian Majwega wa Azam FC akimtoka beki wa Yanga SC Juma Abdul katika mchezo wa jana |
Kabla ya jana, katika Ligi Kuu Yanga walifungwa mara ya mwisho na mahasimu wa jadi, Simba SC Machi 8, mwaka huu 1-0, bao pekee la Emmanuel Okwi.
Kutoka hapo, Yanga SC ilizifunga 2-1 Kagera Sugar, 2-0 Mgambo JKT, 3-1 JKT Ruvu, 8-0 Coastal Union, 3-1 Mbeya City, 3-2 Stand United, 5-0 Ruvu Shooting na 4-1 Polisi Moro.
Pazia la Ligi Kuu linatarajiwa kufungwa mwishoni mwa wiki, Jumamosi kwa mechi saba kupogwa viwanja tofauti; JKT Ruvu Vs Simba SC, Mtibwa Sugar Vs Coastal Union, Stand United Vs Ruvu Shooting, Mbeya City Vs Polisi Moro, Kagera Sugar Vs Prisons, Ndanda FC Vs Yanga SC na Azam FC Vs Mgambo JKT.

.png)
0 comments:
Post a Comment