MABINGWA watetezi, Sevilla wameifunga Fiorentina mabao 3-0 usiku huu wakati Napoli wamelazimishwa sare ya 1-1 na Dnipro katika mechi za kwanza za Nusu Fainali ya Europa League.
Winga wa Kispanyola, Aleix Vidal alifunga mabao katika dakika za 17 na 50 na mshambuliaji wa Ufaransa, Kevin Gameiro akamalizia la tatu Sevilla ikiibuka na ushindi wa tisa mfululizo nyumbani katika michuano ya Ulaya.
Ushindi huo unaiweka Sevilla katika mazingira mazuri ya kutinga fainali ya michuano hiyo Mei 27 mjini Warsaw.
Sevilla iliyoshinda mfululizo Kombe la UEFA mwaka 2006 na 2007, ikibeba na mwaka huu taji hilo, itazifikia Inter Milan, Juventus na Liverpool, zilizoshinda taji hilo mara tatu kila moja.
Mjini Naples, kikosi cha kocha Rafael Benitez, Napoli kilianza kupata bao dhidi ya Dnipro ya Ukraine, wakati David Lopez kufunga dakika ya 52.
Lakini Dnipro, ambao hawajawahi kucheza fainali ya michuano ya Ulaya wakasawazisha dakika ya 81 kupitia kwa Yevhen Seleznyov aliyetokea benchi.
Winga Vidal akishangilia baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Fiorentina usiku huu PICHA ZAIDI NENDA


.png)
0 comments:
Post a Comment