• HABARI MPYA

    Friday, May 08, 2015

    PELE ALAZWA TENA SAO PAULO

    GWIJI wa soka Brazil, Pele mwenye umri wa miaka 74, amelazwa kwa mara ya pili ndani ya miezi sita, hospitalia ya Sao Paulo imesema Alhamisi.
    Msemaji wa hospitali ya Albert Einstein, amethibitisha Pele alikuwa hapo, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi. 
    Tovuti ya Globoesporte ya Brazil imeripoti kwamba Pele alifanyiwa upasuaji Jumanne wa malazi ya nyama za mdomoni zinazoshikilia meno, ambayo tovuti hiyo imesema yanaongeza hatari ya ugonjwa wake wa kibovu cha mkojo.
    Gwiji wa soka duniani,Pele amelazwa kea mara ya tatu ndani ya kmezi sita

    Pele, ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, aliruhusiwa kutoka katika hospitali hiyo hiyo mapema Desemba baada yakulazwa kwa wiki mbili kwa matatizo hayo hayo.
    Akiwa amefunga mabao zaidi ya 1,280 jumla enzi zake anacheza soka, Pele anapewa heshima na mashabki wengi kama mchezaji bora zaidi daima wa dunia kuahi kutokea duniani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PELE ALAZWA TENA SAO PAULO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top