• HABARI MPYA

    Saturday, May 09, 2015

    RUVU SHOOTING NA POLISI MORO ZAIPA MKONO WA KWAHERI LIGI KUU, YANGA WAIBEBA NDANDA

    Ruvu Shooting wameshuka daraja pamoja na Polisi Moro
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU mbili za majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania, Polisi na Ruvu Shooting zimeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo.
    Katika mechi za kufunga pazia la Ligi Kuu leo, Ruvu imefungwa bao 1-0 na wenyeji Stand United mjini Shinyanga, hivyo kumaliza na pointi 29 sawa na Mgambo JKT na Prisons ambazo zimebebwa na wastani mzuri wa mabao.
    Polisi imefungwa 1-0 na Mbeya City hivyo kumaliza na pointi 25, nayo inaungana na Ruvu Shooting kuiaga Ligi Kuu na kuendeleza rekodi yake ya kupanda na kuteremka msimu huo huo.
    Ndanda FC imenusurika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga na kumaliza na pointi 31. 
    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na Prisons, Simba SC imeifunga mabao 2-1 JKT Ruvu, Coastal Union imepata ushindi wa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar mabao 2-1 na Azam FC imetoka sare ya 0-0 na  Mgambo JKT. 
    Wakati Ruvu Shooting na Polisi zikiipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu, tayari Majimaji ya Songea, African Sports ya Tanga, Mwadui ya Shinyanga na Toto Africans ya Mwanza zimepanda.
    Msimu ujao, Ligi Kuu itakuwa na timu mbili zaidi, kutoka 14 hadi 16 ili kuiongezea ushindani na msisimko zaidi. 


    MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA 

                                 P W D L GF GA GD Pts
    1 Yanga SC 26 17 4 5 52 18 34 55
    2 Azam 26 13 10 3 36 18 18 49
    3 Simba SC 26 13 8 5 38 19 19 47
    5 Mbeya City 26 8 10 8 21 23 0 34
    8 Coastal 26 8 10 8 20 26 -4 34
    6 Kagera 26 8 8 10 22 26 -4 32
    4 Mtibwa              26 7 10 9 25 26 -1 31
    7 JKT Ruvu           26 8 7 11 20 25 -5 31
    11 Ndanda 26 8 7 11 21 29 -8 31
    13 Stand Ut           26 6 7 11 22 34 -11 31
    10 Prisons 26 5 14 7 18 22 -4 29
    12 Mgambo          26 8 5 13 18 28 -10 29
    9 Ruvu Shoot 26 7 8 11 16 29 -13 29
    14 Polisi Moro 26 5 10 11 16 27 -11 25
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUVU SHOOTING NA POLISI MORO ZAIPA MKONO WA KWAHERI LIGI KUU, YANGA WAIBEBA NDANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top