MANCHESTER United imeweka hai matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, baada ya jioni ya leo kuilaza mabao 2-1 Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park.
Matokeo hayo yanawafanya Mashetani Wekundu wafikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 36, wakiwa nyuma ya Arsenal wenye pointi 70 mechi 34, Manchester City pointi 70 mechi 35 na mabingwa Chelsea, pointi 83 mechi 35.
Liverpool yenye pointi 61 za mechi 35 ni ya tano, wakati Tottenham Hotspur yenye pointi 58 za mechi 36 ni ya sita.
Juan Mata alianza kuifungia Man United kwa penalti dakika ya 19, baada ya Scott Dann kuunawa mpira wa krosi iliyopigwa na Ashley Young.
Palace ilisawazisha bao hilo dakika ya 57 kupitia kwa Jason Puncheon aliyetokea benchi, baaada ya shuti lake la mpira wa adhabu kumbabatiza kichwani Daley Blind kabla ya kutinga nyavuni.
Marouane Fellaini ndiye aliyeibuka shujaa wa mechi hivi leo, baada ya kuifungia Manchester United bao la ushindi dakika ya 78.
Marouane Fellaini akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Manchester United ikiilaza 2-1 Crystal Palace PICHA ZAIDI GINGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment