• HABARI MPYA

    Saturday, May 09, 2015

    PEP GUARDIOLA AKALIA 'KUTI KAVU' BAADA YA BAYERN MUNICH KUGONGWA MECHI YA NNE MFULULIZO

    'WACHOVU' Bayern Munich wamefungwa bao 1-0 nyumbani na Augsburg katika mechi ya Bundesliga leo, hicho kikiwa kipigo cha nne mfululizo amacho kinakatisha tamaa kuelekea mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Barcelona.
    Bao pekee la Augsburg limefungwa na Raul Bobadilla dakika ya 71 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza daima Uwanja wa Allianz Arena. 
    Kocha Pep Guardiola aliwapumzisha nyota wake kadhaa kwa ajili ya mechi na Barcelona Jumanne, kufuatia kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza Hispania.
    The former Liverpool keeper was show the red card after only 13minutes of the game
    Kipa wa zamani wa Liverpool, Pepe Reina akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 13 tu ya mchezo huo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    VIPIGO MFULULIZO VYA PEP GUARDIOLA BAYERN MUNICH 

    Aprili 28: 1-1 (wakafungwa 2-0 kwa penalti ) na Dortmund (Kombe)
    Mei 2: 0-2 vs Leverkusen (Bundesliga)
    Mei 6: 0-3 vs Barcelona (Ligi ya Mabingwa)
    9 May: 0-1 vs Augsburg (Bundesliga)
    The Bavarians sasa wanapoteza mechi ya nne mfululizo, baada ya vipigo vya awali kutoka kwa Borussia Dortmund katika Kombe la Ujerumani, Bayer Leverkusen katika Ligi na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa wiki hii. 
    Kipa wa pili, Pepe Reina alimchezea rafu mshambuliaji wa Argentina, Bobadilla katika boksi akatolewa kwa kadi nyekundu na kulazimisha kipa wa kwanza, Manuel Neuer aingie. Guardiola sasa amekali 'kuti kavu' Munich kutokana na matokeo haya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PEP GUARDIOLA AKALIA 'KUTI KAVU' BAADA YA BAYERN MUNICH KUGONGWA MECHI YA NNE MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top