• HABARI MPYA

    Friday, May 08, 2015

    HATIMA YA MSUVA NI LEO ‘BONDENI’, YANGA SC WAANZA KUMSAKA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    HATIMA ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva (pichani kushoto) inatarajiwa kujulikana leo katika mpango wake kucheza soka ya kulipwa Afrika Kusini.
    Winga huyo wa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC atafanya majaribio yake ya mwisho leo Bidvest Wits ya Ligi Kuu nchini humo na baada ya hapo, klabu hiyo itaamua kumnunua au la.
    Wakala aliyemuomba Msuva Yanga alisema anampeleka Orlando Pirates kwa majaribio, lakini baada ya kukosa nafasi huko, akamuhamishia Wits University.
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, hadi sasa hawajawasiliana na Msuva tangu aondoke Jumatano.
    “Kama unavyojua, sisi baada ya kuletewa maombi na yule wakala kwamba anataka ampeleke Pirates, tukamuomba (Msuva) asubiri amalize ligi, lakini yeye akatoroka. Na tangu amefika hajawasiliana na sisi. Ila sasa imebidi tuanze kumafuta,” amesema mtangazaji huyo wa zamani wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
    Msuva ametoa mchango mkubwa kwa Yanga SC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu

    Msuva aliondoka akiwa tayari ameipa Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, huku pia akiwa anaongoza kwa mabao, 17 akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Amissi Tambwe mabao 14.   
    Tangu ajiunge na Yanga SC mwaka 2012 akitokea Moro United, Msuva ameifungia timu hiyo mabao 35 jumla katika mechi 102 za mashindano yote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HATIMA YA MSUVA NI LEO ‘BONDENI’, YANGA SC WAANZA KUMSAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top