VIGOGO wa Misri, Zamalek walivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba SC ya Tanzania mwaka 2003 na tangu hapo hawajatwaa taji lolote lingine la Afrika.
Baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2002, Zamalek ilikutana na Simba SC katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa mwaka 2003 na mechi ya kwanza Dar es Salaam, Wamisri hao walilala 1-0 Uwanja wa Taifa.
Katika mchezo wa marudiano, Zamalek wakashinda 1-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti, ambao Simba ilishinda na kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi kwa mara ya kwanza na ya mwisho.
Lakini safari hii, wachezaji na viongozi wa Zamalek wamepania kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika, liwe taji lao la kwanza barani baada ya miaka 13. Zamelek watacheza na SM Sanga Balende ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwania kupangwa katika makundi Kombe la Shirikisho. Vigogo hao wa Misri waliitoa FUS Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 3-2.
Mkurugenzi wa klabu, Ismail Yousef, amesema lengo lao ni kushinda Kombe la Shirikisho mwaka huu. “Tunazikaribisha timu zote. Tuko tayari kucheza dhidi ya timu yoyote, kwani tuna ndoto ambayo ni kushinda Kombe la Shirikisho, hivyo hatujali tutacheza na nani," amesema Yousef.
Mshambuliaji wa Zamalek, Ahmed Ali amesema kwamba Sanga Balende si timu kubwa, lakini wanapaswa kuwaheshimu Wakongo hao.
Zamalek itacheza mechi ya kwanza DRC Mei 15, 16 au 17 wakati marudiano yatakuwa Cairo wiki ya kwanza ya Juni.

![]() |
| Zamalek hawajatwaa taji lolote barani tangu wavuliwe ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2003 na Simba SC |
Lakini safari hii, wachezaji na viongozi wa Zamalek wamepania kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika, liwe taji lao la kwanza barani baada ya miaka 13. Zamelek watacheza na SM Sanga Balende ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwania kupangwa katika makundi Kombe la Shirikisho. Vigogo hao wa Misri waliitoa FUS Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 3-2.
Mkurugenzi wa klabu, Ismail Yousef, amesema lengo lao ni kushinda Kombe la Shirikisho mwaka huu. “Tunazikaribisha timu zote. Tuko tayari kucheza dhidi ya timu yoyote, kwani tuna ndoto ambayo ni kushinda Kombe la Shirikisho, hivyo hatujali tutacheza na nani," amesema Yousef.
Mshambuliaji wa Zamalek, Ahmed Ali amesema kwamba Sanga Balende si timu kubwa, lakini wanapaswa kuwaheshimu Wakongo hao.
Zamalek itacheza mechi ya kwanza DRC Mei 15, 16 au 17 wakati marudiano yatakuwa Cairo wiki ya kwanza ya Juni.

.png)
0 comments:
Post a Comment