• HABARI MPYA

    Friday, May 08, 2015

    BENTEKE AWAANGUSHA JOHN TERRY NA ANDER HARRERA TUZO YA MCHEZAJI BORA ENGLAND

    MSHAMBULIAJI Christian Benteke ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza Aston Villa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England, tangu Ashley Young abebe tuzo hiyo Desemba mwaka 2008 kabla ya kuhamia Manchester United.
    Benteke, ambaye ameisaidia Aston Villa kuiacha kwa pointi mbili Sunderland inayoshika nafasi ya 18 katika msimamo wa Ligi Kuu, mabao yake ndiyo yamempa tuzo ya Mchezaji Bora wa Aprili, akiwapiku John Terry wa Chelsea na Ander Herrera wa Man United.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Manchester United na Liverpool wiki za karibuni, mwezi uliopita alifunga mabao matano katika mechi nne.
    Christian Benteke proudly shows off his Premier League Player of the Year Award for April
    Christian Benteke akifurahia na tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England mwezi Aprili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENTEKE AWAANGUSHA JOHN TERRY NA ANDER HARRERA TUZO YA MCHEZAJI BORA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top