• HABARI MPYA

  Monday, January 19, 2015

  SIMBA WA TERANGA WATAFUNA WAGHANA AFCON

  SIMBA wa Teranga, Senegal wameifunga Ghana mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi C Fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea Equatorial Guinea.
  Sifa zimuendee Moussa Sow aliyetokea benchi na kufunga bao la ushindi.
  Sow alifumua shuti akipiga mpira wa mwisho kabla ya filimbi ya kumaliza mchezo na kufunga bao la ushindi, baada ya Mame Biram Diouf kusawazisha bao la mapema la Black Stars lililofungwa na Andrew Ayew kwa penalti.Sow screams in celebration after stealing three points for Senegal against Ghana in the AFCON 2015
  Moussa Sow akishangilia baada ya kuifungia Senegal bao la ushindi dhidi ya Ghana AFCON 2015

  Hayo ni matokeo machungu kwa kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant katika mchezo wake wa kwanza akiwa kazini Ghana, ambayo sasa yanawaweka mabingwa hao wa zamani katika mazingira magumu kuingia hatua ya 16 Bora.
  Algeria na Afrika Kusini ni timu nyingine kwenye kundi hilo, ambazo zinamenyana baadaye usiku huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WA TERANGA WATAFUNA WAGHANA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top