• HABARI MPYA

  Monday, January 19, 2015

  YANGA SC WAHAMIA UWANJA MBOVU ILI…

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga kimelazimika kuhamishia mazoezi yake Uwanja ‘mbovu’ wa Tanganyika Parkers, kwa sababu mechi ijayo watacheza kwenye Uwanja wa aina hiyo.
  Kocha Mkuu wa Yanga Hans Pluijm ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba kwamba wamelazimika kuhamia Uwanja wa Tanganyika Packers kufuatia eneo hilo kufanana na Uwanja wa Jamhuri uliopo Mkoani Morogoro ambao ndiyo mchezo wao dhidi ya Polisi utapigwa Januari 24.
  Pluijm alisema wameshindwa kuendelea kuutumia Uwanja wa kisasa wa Boko Veterani kutokana na kuwa na utofauti mkubwa na ule wa Jamhuri.
  Mrisho Ngassa akimiliki mpira mbele ya Nadir Haroub 'Cannavaro' leo Tanganyika Packers
  Kpah Sherman mbele ya Oscar Joshua leo mazoezini katika Uwanja mbovu

  Amesema anataka wachezaji wake wazoee kucheza Uwanja mbovu ili wasipate tabu katika mchezo wao na Polisi.
  "Kuanzia leo tutakuwa tunafanyia hapa mazoezi, ukiangalia hiki kiwanja sio kizuri sana ni kuibovu kama kile cha Jamhuri ambacho tutachezea mechi yetu dhidi ya Polisi,"alisema Pluijm.
  "Hatuwezi kufanya mazoezi katika uwanja mzuri na baadaye tukacheze mechi katika uwanja mbovu hili litawapa shida wachezaji, "amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAHAMIA UWANJA MBOVU ILI… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top