• HABARI MPYA

  Monday, January 19, 2015

  RANGERS YAFUFUA MATUMAINI YA LIGI KUU

  TIMU ya Friends Rangers imepata ushindi wa bao 1-0 dhisi ya Polisi Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja Karume, Dar es Salaam. 
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, John Joseph dakika ya 25 na sasa Rangers inatimiza pointi 32 baada ya kucheza mechi 18, ingawa inabaki nafasi ya tatu katika Kundi A.
  Majimaji inaongoza kwa pointi zake 36 za mechi 17, ikifuatiwa na African Sports yenye pointi 35 mechi 17 pia.
  Matokeo mengine ya michezo ya leo Daraja la Kwanza, JKT Mlale imeifunga 2-0 African Lyon na KMC imetoka sare ya bila kufungana na Ashanti United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RANGERS YAFUFUA MATUMAINI YA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top