• HABARI MPYA

  Tuesday, January 06, 2015

  PLUIJM, MKWASA WAKISOMA MBINU ZA SIMBA SC

  Makocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm (kushoto) na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa kulia wakishuhudia mchezo wa Kundi C Kombe la Mapinduzi kati ya Simba SC na JKU Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku wa jana. Simba SC ilishinda 1-0 na kutinga Robo Fainali. Yanga inaweza kukutana na Simba SC katika michuano hiyo. Makocha kadhaa wamefukuzwa Yanga SC kwa sababu ya kufungwa na Simba SC na Pluijm katika kulitambua hilo amekuwa akihudhuria mechi zote za mahasimu wao ili kusoma mbinu zao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM, MKWASA WAKISOMA MBINU ZA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top