• HABARI MPYA

  Friday, January 09, 2015

  NAHODHA WA COASTAL UNION NA WENGINE 15 WAHAMIA GOR MAHIA

  Wachezaji wapya wa Gor Mahia, Jerry Santo wa kwanza kushoto waliosimama

  WACHEZAJI WAPYA WA GOR MAHIA 

  Jerry Santo – kiungo kutoka Coastal Union
  David Onyango Magoma – mshambulizi kutoka Mawego Talent Academy
  Ali Abondo "Teargas' – kiungo kutoka Tusker FC
  Ronald Otieno Omino – straika kutoka Muhoroni Youth
  Earnest Wendo – kiungo mkabaji kutoka Bidco United
  Farouk Ssentongo – kiungo mshambulizi kutoka Uganda
  James Ohawa – straika kutoka Bombo FC ya Uganda
  Augustine Walusimbi – beki kutoka Masaka Local Council FC
  Dirkir Glay – beki kutoka Thika United
  Zachary Toufiq – straika kutoka Ghana
  Khalid Aucho – kiungo kutoka Tusker FC
  Martin Werunga – beki kutoka FC Talanta,  
  Michael Olunga straika kutoka Thika United, 
  Innocent Wafula –kiungo kutoka Chemelil Sugar
  Boniface Oluoch – kipa kutoka Tusker FC
  Bernard Odhiambo – beki kutoka Nakuru AllStars 
  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  ALIYEKUWA nahodha wa Coastal Union ya Tanzania bara na mkenya Jerry Santo ni miongoni mwa wachezaji kumi na sita waliozinduliwa na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia.
  Gor imo mbioni kujiandaa kombe la klabu bingwa barani Afrika na sasa imewasajili wachezaji kumi na sita kujaza nafasi za wachezaji walioondoka miongoni mwao Dan Sserunkuma aliyehamia Simba SC, Geoffrey ‘Baba’ Kizito kwenda Vietnam na David ‘Calabar’ Owino aliyejiunga na ZESCO United ya Zambia.
  Sasa Gor Mahia ina jumla ya wachezaji 28 na wanayo nafasi mbili kufanya sajili nyingine. 
  Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zasema kuwa wana mikakati ya kumnasa straika la mahasimu wao wa jadi AFC Leopards Jacob Keli na vile vile nahodha wa Muhoroni Youth Abbas Akinyemi.
  Misimu miwili iliyopita, Santo aling'ara na Coastal Union ya Tanga katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, hiyo ni klabu ya pili kuchezea nchini humo baada ya awali kuwa Simba SC ya Dar es Salaam.
  Kabla ya kurejea Kenya, Santo alijaribu kurejea Simba SC, lakini hakufanikiwa kutokana na kugoma kufanya majaribio kama alivyotakiwa na kocha wa Wekundu hao wakati huo, Mcroatia Zdravko Logarusic. Santo pia alikwenda Oman kujaribu kujiunga na Fanja ya huko bila mafanikio na hatimaye sasa amerudi nyumbani kujipanga upya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAHODHA WA COASTAL UNION NA WENGINE 15 WAHAMIA GOR MAHIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top