// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STARS NA RWANDA KUCHEZA MWANZA JANUARI 22 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STARS NA RWANDA KUCHEZA MWANZA JANUARI 22 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, January 09, 2015

    STARS NA RWANDA KUCHEZA MWANZA JANUARI 22

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Taifa Stars Maboresho kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
    Mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij (pichani kushoto) kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN). Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.
    Kocha Nooij anatarajia wakati wowote kutangaza kikosi cha timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kitakusanyika Januari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na siku moja baadaye kwenda jijini Mwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS NA RWANDA KUCHEZA MWANZA JANUARI 22 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top