// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MABOSI WA ARSENAL WAWASILI DAR NA HABARI NJEMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MABOSI WA ARSENAL WAWASILI DAR NA HABARI NJEMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, January 20, 2015

    MABOSI WA ARSENAL WAWASILI DAR NA HABARI NJEMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAOFISA wa klabu ya Arsenal ya England wamewasili mjini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano na wafanyabiashara kadhaa wakubwa nchini Tanzania.
    Huu unakuwa ujumbe wa kwanza kabisa wa Arsenal nchini Tanzania, ambapo klabu hii kubwa ya Uingereza inataka kujenga ushirika mkubwa kabisa katika maeneo ya masoko na chapa zake, ili kutanua mafanikio yaliyofikiwa kwenye nchi nyingine za Afrika kama Kenya, Uganda na Nigeria.
    Washika Bunduki hao wa London wanataka kutoa fursa kwa benki za Tanzania pamoja na kampuni za simu na taasisi nyingine kuweza kupata rasilimali zihusianazo na Arsenal, kama vile bidhaa zilizosainiwa kwa majina ya wachezaji, tiketi za mechi.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula (kushoto) akizunguma na Meneja Maendeleo wa Arsenal, Daniel Willey (kulia) jana

    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula (kushoto), Meneja Maendeleo wa Arsenal, Daniel Willey (kulia) na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Arsenal, Sam Stone.  

    Maofisa hao wa Arsenal wanasema kwamba wanaweza kuwapatia washirika wao hao uwanja mpana wa masoko kwa ajili ya kuwasaidia kutimiza malengo mbalimbali ya kibiashara.
    Ofisa Biashara Mkuu wa Arsenal, Vinai Venkatesham amesema kwamba wameichagua Tanzania kwa sababu wana mashabiki wengi, na kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania, watakuwa karibu zaidi na washabiki wao kuliko ilivyokuwa awali.
    "Katika bara lenye nchi zaidi ya 50, tumechagua kuzuru Tanzania kimkakati kwa sababu tunaiamini nchi hiyo. Arsenal ina mamilioni ya Watanzania ambao ni washabiki waaminifu na wenye mapenzi makubwa nayo,”.
    "Kwa kushirikiana na taasisi za huko, tutaweza kuisogeza klabu karibu zaidi na washabiki hao kuliko ilivyokuwa awali, huku tukizipatia taasisi husika fursa pekee za kuifikia klabu yetu," akasema Venkatesham.
    Wajumbe hao wa jopo la Maendeleo ya Ushirikiano ya Arsenal watakuwa nchini kwa wiki moja wakifanya mikutano kadhaa ya awali ya kibiashara na kuzindua rasmi mchakato wa kutafuta washirika wa kwanza kabisa nchini Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABOSI WA ARSENAL WAWASILI DAR NA HABARI NJEMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top