• HABARI MPYA

  Tuesday, January 20, 2015

  MWAPE WA YANGA ATUPIWA VIRAGO ZAMBIA, ZANACO YAFUKUZA NA MAKOCHA

  Na Mwandishi Wetu, LUSAKA
  KLABU ya Zanaco FC imemtema mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC ya Tanzania na Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Davies Mwape huku Aubrey Zulu ikimrudisha Choma Eagles.
  Klabu hiyo imeleta Wanigeria wanne kwa ajili ya majaribio ambayo wataanza sambamba na maandalizi ya Zanaco ya msimu mpya, Januari 22 mjini Lusaka.
  Pamoja na hayo, timu hiyo mabadiliko ya benchi lake la Ufundi, kuelekea msimu wa Ligi Kuu ya nchi hiyo, ikimuhamishia Aggrey Chiyangi kwenye Ushauri wa Ufundi.
  Davies Mwape ametemwa Zanaco ya nyumbani kwao Zambia

  Nafasi ya Chiyangi imechukuliwa na Msaidizi wa pili wa muda mrefu, Mumamba Numba, ambaye amekuwa kazini tangu mwanzoni mwa mwaka 2014 baada ya timu hiyo ya Lusaka kushindwa kumpa Mkataba mpya, Keagan Mumba.
  Chiyangi amekuwa na matokeo yasiyoridhisha kwa mabingwa hao mara sita wa Zambia, huu ukiwa mwaka wa pili mfululizo.
  Zanaco ilishindwa kushika nafasi mbili za juu katika msimu wa 2014 baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu ikiziwa pointi mbili na Zesco United yaaani 57 kwa 59.
  Zanaco ilimaliza nafasi ya tano mwaka 2013 na kutemeshwa ubingwa wa Ligi Kuu ya FAZ waliotwaa mwaka 2012 chini ya marehemu Mumba.
  Wakati huo huo, Zanaco Msaidizi wa kwanza wa Chiyangi, John Lungu wakati Kalumba Mpunga na Robin Munsaka wamepandishwa kutoka timu ya vijana, Young Zanaco na watakuwa Wasaidizi wa Numba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAPE WA YANGA ATUPIWA VIRAGO ZAMBIA, ZANACO YAFUKUZA NA MAKOCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top