• HABARI MPYA

  Tuesday, January 06, 2015

  COUTINHO AWANIA KUMPIKU MSUVA UFUNGAJI BORA KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  KIUNGO Mbrazil wa Yanga SC, Andrey Coutinho, ameingia kwenye mbio za kuwania ufungaji bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kufunga bao lake la tatu leo.
  Coutinho ameifungia Yanga SC bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Shaba mchezo wa mwisho wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Yanga SC imemaliza na pointi tisa na mabao tisa ya kufunga, kati ya hayo, matatu amefunga Coutinho, manne Simon Msuva na mawili Mliberia, Kpah Sherman. Haijafungwa hata bao moja.

  Andrey Coutinho anawania ufungaji bora Kombe la Mapinduzi baada ya kufikisha mabao matatu leo

  WANAOWANIA UFUNGAJI BORA KOMBE LA MAPINDUZI 2015

  Simon Msuva  Yanga 4
  Andy Coutinho Yanga  3   
  William Wadri KCCA  3        
  Amour Omary JKU   2
  Kpah Sherman  Yanga  2       
  Msuva ndiye anayeongoza kwa mabao katika michuano ya mwaka huu hadi sasa, akifuatiwa na William Wadri wa KCCA na Coutinho wenye mabao matatu kila mmoja, wakati Amour Omary wa JKU na Sherman wana mabao mawili kila mmoja.
  Michuano hiyo imefikia katika hatua Robo Fainali ambazo zitaanza kesho Saa 2:15 Usiku Uwanja wa Amaan, Simba SC ikimenyana na Taifa ya Jang’ombe.
  Keshokutwa Yanga SC itamenyana na JKU, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya KCCA na Polisi Saa 9:00 Alasiri, Azam FC na Mtibwa Sugar Saa 11:00.
  Kwa mujibu wa Ratiba ya mashindano haya, Nusu Fainali zitachezwa Januari 10 Uwanja wa Amaan, ambazo zitawakutanisha mshindi kati ya Simba na Taifa dhidi ya mshindi kati ya KCCA ya Uganda na Polisi Zanzibar na mshindi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar dhidi ya mshindi kati ya Yanga na JKU.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COUTINHO AWANIA KUMPIKU MSUVA UFUNGAJI BORA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top