• HABARI MPYA

    Thursday, November 06, 2014

    MESSI AMFIKIA RAUL KWA MABAO ULAYA, BARCA IKIICHAPA 2-0 AJAX

    WAFUNGAJI WA KIHISTORIA LIGI YA MABINGWA ULAYA 

    1: Lionel Messi (Barcelona)  na Raul (Real Madrid, Schalke) kila mmoja mabao 71
    3: Cristiano Ronaldo (Manchester United, Real Madrid) - Mabao 70
    4: Ruud van Nistelrooy (PSV Eindhoven, Manchester United, Real Madrid) Mabao 56
    5: Thierry Henry (Monaco, Arsenal, Barcelona) - Mabao 50
    MSHAMBULIAJI Lionel Messi ameifikia idadi ya mabao aliyofunga Raul katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga lake la 71 jana.
    Nyota huyo wa Barcelona alifunga mabao mawili dhidi ya Ajax katika ushindi wa 2-0 na sasa anaongoza kwa pamoja na gwiji huyo wa Real Madrid kufunga mabao kwenye michuano hiyo.
    Messi, nyota wa vigogo wa Katalunya ili kukamata rekodi hiyo iliyowekwa muongo uliopita, alifunga bao la kwanza kwa kichwa, kabla ya kuongeza la pili kipindi cha pili Barcelona katika mchezo huo wa Kundi F. Pamoja na kushinda, Barca inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake tisa, nyuma ya PSG yenye pointi 10 baada ya kuifunga APOEL Nicosia 1-0.
    Lionel Messi akishangilia baada ya kuifikia rekodi ya mabao ya Raul usiku wa kuamkia leo

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2822355/Lionel-Messi-equals-Raul-s-time-Champions-League-goalscoring-record-brace-Barcelona.html#ixzz3IFWOgZbM 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI AMFIKIA RAUL KWA MABAO ULAYA, BARCA IKIICHAPA 2-0 AJAX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top