KLABU ya Manchester United inamfuatilia mshambuliaji kinda wa Brazil, Douglas Coutinho.
Wawakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 wanatarajiwa kusafiri hadi Ulaya wiki ijayo kuzungumzia mustakabli wa kinda huyo.
Monaco na Atletico Madrid nazo zinamtaka mchezaji huyo zikiwa zimetoa ofa ya Pauni Milioni 7.5.
Manchester United intake kusajili mshambuliaji kinda wa Brazil, Douglas Coutinho kutoka Atletico Paranaense
Wasaka vipaji wa United wamekuwa na kawaida ya kuangalia michezo ya Brazil na wan a mawasiliano mazuri na baadhi ya klabu. Mshambuliaji huyo wa Atletico Paranaense, Coutinho amefunga mabao saba katika mechi 25 hadi sasa mwaka huu.
Coutinho yuko ndani ya Mkataba hadi mwaka 2017 na anaweza kuondoka Atletico kwa sababu inakabiliwa na hali mbaya kiuchumi.
Mkataba wa sasa wa Coutinho unatarajiwa kumalizika mwaka 2017 Atletico
0 comments:
Post a Comment