• HABARI MPYA

    Friday, November 14, 2014

    LIVERPOOL TAYARI KUTOA 'CHA JUU' ILI IMPATE ORIGI JANUARI

    KLABU ya Liverpool inajiandaa kuongeza dau kutoka Pauni Milioni 10 ilizokubaliana na Lille ili kumpata mshambuliaji Divock Origi ifikapo Januari.
    Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, ambaye Brendan Rodgers anaamini mshambuliaji wa kiwango cha dunia, alijiunga na Liverpool mwezi Agosti, lakini akarudishwa kwa mkopo Lille ili kupata uzoefu zaidi kabla ya kwenda kuanza kazi Anfield msimu ujao.
    Lakini kwa kuwa sasa Liverpool inamhitaji Origi, na wake tayari kutoa cha juu. Timu ya Rodgers kwa sasa ina tatizo la safu ya ushambuliaji katokana na Daniel Sturridge kukosa mechi 14 kwa sababu ya majeruhi, huku Rickie Lambert, Mario Balotelli na Fabio Borini wakishindwa kukidhi mahitaji ya mabao katika timu.
    Belgium's Divock Origi, second left, scores the second goal against Iceland on Wednesday night
    Mbelgiji Divock Origi, wa pili kushoto, alifunga bao la pili dhidi ya Iceland juzi
    Origi (right) celebrates with team-mates after his goal against Iceland at the King Baudouin stadium
    Origi (kulia) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga dhidi ya Iceland Uwanja wa King Baudouin

    Pamoja na hayo, Lille haijapewa taarifa yoyote juu ya kumuachia Origi aende Liverpool mapema, ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 amesema atafurahia kuhamia Januari.
    "Si mimi ninayefanya maamuzi, lakini ikiwa klabu itachaguao kuniruhusu Januari nitakwenda, ningependa kujiunga na Liverpool," amesema Origi, ambaye bao katika ushindi wa 3-1 wa Ubelgiji dhidi ya Iceland.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL TAYARI KUTOA 'CHA JUU' ILI IMPATE ORIGI JANUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top