• HABARI MPYA

    Saturday, October 11, 2014

    'RVP' APIGA BAO UHOLANZI IKITOA ADHABU KUFUZU EURO

    NAHODHA Robin van Persie ameifungia Uholanzi ikipata ushindi wa kwanza katika mechi tatu chini ya kocha Guus Hiddink tangu arithi mikoba baada Louis Van Gaal, baada ya kuifunga Kazakhstan mabao 3-1 katika mechi ya Kundi A kufuzu Euro 2016. 
    Kazakhstan walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Rinat Abdulin dakika ya 18 kabla ya Klaas-Jan Huntelaar kusawazisha dakika ya 62.
    Wageni walipata pigo baada ya mchezaji wao, Bauyrzhan Dzholchiev kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumchezea rafu Ibrahim Afellay dakika ya 64.
    Afellay akaifungia Uholanzi bao la pili dakika ya 82 kabla ya Robin van Persie ‘kuunenepesha’ ushindi kwa bao la dakika ya 89 kwa penalti.  Katika mechi nyingine za Kundi A, Iceland imepata ushindi wa ugenini wa 3-0 dhidi ya Latvia na Jamhuri ya Czech imeshinda ugenini pia 2-1 dhidi ya Uturuki.
    Robin Van Persie akipongezwa baada ya kufunga bao la tatu jana

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'RVP' APIGA BAO UHOLANZI IKITOA ADHABU KUFUZU EURO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top