• HABARI MPYA

    Tuesday, October 07, 2014

    PHIRI AMJIBU MAXIMO; “YANGA SC IPO KWENYE KIGANJA CHO MKONO WANGU”

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Simba SC, Mzambia, Patrick Phiri amesema kwamba anaijua vizuri Yanga SC na kuelekea mpambano baina yao Oktoba 18, hana wasiwasi hata chembe.
    Phiri amesema kwamba aliuangalia vizuri mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC ikifungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro na akaangalia mchezo mwingine, wakiifunga Azam FC 3-0.
    “Kwa mechi hizi mbili imetosha kuijua Yanga SC, inatosha kwangu kwa kujipanga kwa ajili ya mechi na wao na sina wasiwasi hata kidogo,”amesema Phiri akihojiwa na BIN ZUBEIRY jana.
    Kocha wa Simba SC, Mzambia Patrick Phiri amesema hana wasiwasi na Yanga SC kuelekea mpambano wao wa Oktoba 18, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 

    REKODI YA PATRICK PHIRI TANGU AREJEE SIMBA AGOSTI 2014 

    Simba SC 2-1 Kilimani City (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 2-0 Mafunzo (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 5-0 KMKM (Kirarfiki, Zanziabr)
    Simba SC 3-0 Gor Mahia (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Simba SC 0-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Simba SC 0-0 Ndanda (Kirafiki Mtwara)
    Simba SC 2-2 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Polisi Moro (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Stand United (Ligi Kuu)
    Hata hivyo, Mzambia huyo amesema kwamba kwa sasa kitu muhimu zaidi ni kutatua matatizo yaliyopo ndani ya Simba SC na si kuanza kuifikiria Yanga SC.
    “Tuna matatizo ndani ya Simba SC, hicho ndiyo kitu cha kwanza nitaanza kufanyia kazi katika maandalizi yetu, baada ya hapo ndipo tutawaangalia Yanga wanachezaje,”amesema.
    Simba SC inaanza mazoezi leo baada ya mapumziko ya siku mbili tangu icheze na Stand United Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare ya 1-1.
    Hiyo ilikuwa ni sare ya tatu mfululizo kikosi cha Kocha Patrick Phiri katika mechi zote tatu za mwanzo za Ligi Kuu, baada ya awali kutoka 2-2 na Coastal Union na 1-1 pia na Polisi Moro.
    Sare huzo mfululizo hakika zimewashitua viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na hata wapenzi na mashabiki wa Simba, hususan timu ikielekea katika mchezo na mahasimu, Yanga SC Oktoba 18.
    Phiri aliyerejea Simba SC Agosti mwaka huu kurithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyefukuzwa- hadi sasa amekwishaiongoza timu hiyo katika mechi tisa, kati ya hizo akishinda nne kufungwa moja na sare nne. 
    Jana, kocha wa Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo alikaririwa na BIN ZUBEIRY akisema kwamba hawahofii Simba SC kuelekea mchezo huo- ingawa anawahehimu kama timu nzuri na kongwe. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PHIRI AMJIBU MAXIMO; “YANGA SC IPO KWENYE KIGANJA CHO MKONO WANGU” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top