Emmanuel Okwi kesho anatarajiwa kuiongoza Uganda dhidi ya Togo Uwanja wa Mandela, Kampala, katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kabla ya timu hizo kurudiana Jumatano mjini Lome
MZUNGUKO wa kwanza wa hatua ya makundi, mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco unafikia tamati wikiendi hii.
Botswana watakuwa wenyeji wa Misri mchezo wa Kundi G, Guinea na Ghana mjini Conakry mchezo wa kundi E, Lesotho na Angola mchezo wa Kundi C, Sierra Leone na Cameroon Kundi D na Senegal na Tunisia Kundi G.
Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuiongoza Uganda, The Cranes dhidi ya Togo kesho mjini Kampala katika mchezo wa Kundi E.
Malawi itamenyan na Algeria, Ethiopia na Mali, Msumbiji na Cape Verde, Kongo na Afrika Kusini, DRC na Ivory Coast, Niger na Zambia, Sudan na Nigeria na Gabon na Burkina Faso.
Mechi za kwanza za mzunguko wa pili, zinatarajiwa kuanza Jumatano kwa timu zinazocheza nyumbani wikiendi hii kuwafuata wapinzani wao katikati ya wiki. Uganda watasafiri kuifuata Togo siku hiyo mjini Lome.
0 comments:
Post a Comment