• HABARI MPYA

    Friday, October 10, 2014

    LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA KUTIMUA VUMBI

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    LIGI Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) msimu wa 2014/2015 inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 11 mwaka huu) katika viwanja tisa tofauti kwenye miji ya Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza, Geita, Mbozi, Songea, Mufindi na Dar es Salaam.
    Kundi A litakuwa na mechi kati ya Kimondo FC na Villa Squad itachezwa Uwanja wa Vwawa mjini Mbozi wakati Majimaji itaumana na Ashanti United (Uwanja wa Majimaji, Songea).
    Kikosi cha Toto Africans 

    Nyingine ni Kurugenzi Mafinga na Tessema FC kwenye Uwanja wa Mufindi huku Friends Rangers ikioneshana kazi na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
    Kundi B ni Panone itaikabili Kanembwa JKT (Uwanja wa Ushirika, Moshi), Oljoro JKT itapambana na Polisi Dodoma (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abedi, Arusha), Polisi Mara na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Musoma).
    Mechi nyingine ni kati ya Toto Africans na Mwadui itakayofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Geita Gold na Burkina Faso (Uwanja wa Waja, Geita).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA KUTIMUA VUMBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top