• HABARI MPYA

    Sunday, October 05, 2014

    MTIBWA SUGAR YAIENGUA AZAM FC KILELENI, YASHINDA MECHI YA TATU MFULULIZO

    MTIBWA Sugar imeiengua Azam FC kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mgambo ya Tanga Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro jioni ya leo.
    Matokeo hayo, yanaifanya timu ya Mecky Mexime Kianga itimize pointi tisa baada ya mechi tatu, awali ikizifunga Yanga SC 2-0 na Ndanda FC 3-1.  
    Bao lililoipandisha kileleni Mtibwa Sugar leo limefungwa na Ally Shomary dakika ya 10 ya mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
    Azam FC ipo nafasi ya pili kwa pointi zake saba ilizovuna katika ushindi wa mechi mbili 3-1 na Polisi Moro, 2-0 na Ruvu Shooting na sare ya 0-0 na Prisons jana mjini Mbeya.
    Kileleni; Mtibwa Sugar wamepaa kileleni mwa Ligi Kuu leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAIENGUA AZAM FC KILELENI, YASHINDA MECHI YA TATU MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top