Na Renatus Mahima, MBEYA
MCHEZAJI wa Mbeya City, Anthony Matogolo amewashukuru kocha wake, Juma Mwambusi na wachezaji wenzake kwa ushirikiano wanaompa hadi amekuwa mchezaji bora Septemba katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Beki huyo ametoa shukrani hizo baada ya jana kukabidhiwa zawadi ya Sh Milioni 1 na wadhamini, Vodacom Tanzania Uwanja wa Sokoine, Mbeya. “Ninawashukuru kocha na wachezaji wenzangu wa Mbeya City kwa ushirikiano wanaonipa, hii ni zawadi kwa timu nzima na mashabiki wa
timu yetu,”alisema.
Makabidhiano hayo yalifanyika muda mfupi kabla ya mechi ya raundi ya nne kati ya Mbeya City na Azam FC iliyoshinda 1-0, bao pekee la beki Aggrey Morris.
Kabla ya kukabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Vodacom Tanzania Kanda ya Mbeya, Emmanuel Sagenge, alisema kampuni hiyo itakuwa ikitoa zawadi kila mwezi kwa mchezaji anayefanya vizuri.
Matogolo amekuwa mwenye bahati ya aina yake kuteuliwa Mchezaji Bora wa Septemba, kwani takwimu za kitaalamu hazikumpa nafasi hiyo.
Bodi ya Ligi imeonyesha haiko makini kuipeleka tuzo kwa mchezaji ambaye hakustahili kulingana na takwimu za kitaalamu.

![]() |
Anthony Matogolo akiinua tuzo yake juu baada ya kukabidhiwa jana |
Makabidhiano hayo yalifanyika muda mfupi kabla ya mechi ya raundi ya nne kati ya Mbeya City na Azam FC iliyoshinda 1-0, bao pekee la beki Aggrey Morris.
Kabla ya kukabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Vodacom Tanzania Kanda ya Mbeya, Emmanuel Sagenge, alisema kampuni hiyo itakuwa ikitoa zawadi kila mwezi kwa mchezaji anayefanya vizuri.
Matogolo amekuwa mwenye bahati ya aina yake kuteuliwa Mchezaji Bora wa Septemba, kwani takwimu za kitaalamu hazikumpa nafasi hiyo.
Bodi ya Ligi imeonyesha haiko makini kuipeleka tuzo kwa mchezaji ambaye hakustahili kulingana na takwimu za kitaalamu.
0 comments:
Post a Comment