• HABARI MPYA

    Thursday, June 05, 2014

    WALIOITOA MBEYA CITY WAWA MABINGWA MICHUANO MIPYA YA CECAFA

    Na Rogers Mulindwa, KHARTOUM
    TIMU ya Victoria University ya Uganda imetwaa ubingwa wa michuano mipya ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nile Basin iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu nchini Sudan baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya mabao 2-1 kwenye Fainali Uwanja wa kimataifa wa Khartoum usiku wa jana. 
    Waganda hao walioitoa Mbeya City ya Tanzania katika Robo Fanali kwa bao 1-0, kwa ushindi huo wamezawadiwa dola za Kimarekani 30,000, takriban Sh. Milioni 50 za Tanzania.
    Nahodha wa Victory University,Martin Mpunga akipokea Kombe kutoka kwa Wazii wa Vijana na Michezo wa Sudan, Yahia Hamad jana.

    Washindi wa pili, Leopards wanarejea nyumbani na dola 20.000 wakati  wenyeji Ahly Shandy walioifunga Academie Tchite ya Burundi mabao 4-1 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, wamepata dola 10,000.
    Mabao ya Victoria University katika fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA au washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama wa CECAFA yamefungwa na Odongo Mathew dakika ya 29 na Mutyaba Muzamir dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90, wakati bao la Leopards lilifungwa na Ikene Austin dakika ya 45.
    Mchezaji wa Victory University, Dennis Okoth akimpiga tobo beki wa Leopards, Abdallah Juma jana

    Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, Academie Tchite ilitangulia kupata bao kupitia kwa Bivakumana Jimmy dakika ya 17, lakini Shandy ikatoka nyuma na kushinda kwa mabao ya Eltayb Nadir dakika ya 48, Mohiad Khalid dakika ya 61, Addis Hintsa dakika ya 69 na Elnaeen Mohamed dakika ya 75. Bado haijajulikana nani atakuwa mwenyeji wa pili wa michuano hiyo mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WALIOITOA MBEYA CITY WAWA MABINGWA MICHUANO MIPYA YA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top