// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SERIKALI YAIAGIZA TRA IISHUGHULIKIE TFF YA MALINZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SERIKALI YAIAGIZA TRA IISHUGHULIKIE TFF YA MALINZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 05, 2014

    SERIKALI YAIAGIZA TRA IISHUGHULIKIE TFF YA MALINZI

    Na Renatus Mahima, DODOMA
    SERIKALI imeigiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuliamuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutumia mfumo wa tiketi za elektroniki (ETS) kwenye viwanja mbalimbali vya soka nchini ili kudhibiti uhujumu wa mapato ya milangoni.
    Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara kuhusu utelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa mwaka wa fedha 2014/15 Bungeni mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Luhaga Mpina ameitaka TRA kutoa sharti kwa TFF kutumia mfumo wa tiketi za elektroniki ili kuongeza mapato ya nchi.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi sasa atapambana na TRA katika mfumo wa tiketi za Elektroniki

    "Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inashauri TRA iweke sharti la lazima la kuitaka TFF kutumia mfumo wa tiketi za elektroniki katika kuuza tiketi zake ikiwa ni jitihada za kuongeza mapato ya serikali," amesema Mpina.
    Mbunge huyo wa Kisesa (CCM), amesema kwa muda mrefu serikali imekuwa haipati mapato ya kutosha kutoka katika sekta ya michezo hususani mpira wa miguu ulio chini ya TFF kutokana na mfumo dhaifu wa ukusanyaji fedha kipindi cha kuuza tiketi.
    "Serikali haipati mapato ya kutosha kutokana na mpira wa miguu kwa sababu ya tiketi bandia kuendelea kutumika, kukosekana kwa uwazi katika mapato halisi, uwezo mdogo wa kusambaza tiketi nchi nzima na rushwa kwenye mageti ya viwanja," amesema.
    "Hali hii inaifanya TRA ishindwe kukusanya mapato halisi katika sekta hii na hata katika upande wa klabu na wachezaji hawanufaiki ipasavyo, kwani fedha nyingi hubaki mifukoni mwa wajanja wachache.
    "TFF iliona changamoto hizi na kuamua kutangaza zabuni ya tiketi ETS mwaka 2012 na Benki ya CRDB ilishinda na tayari imekwishatayarisha na kuweka mfumo huo kwa gharama ya Sh. bilioni tatu toka mwaka 2013, na kwenye viwanja vya Kaitaba, Mkwakwani, Azam Complex, Sokoine, Jamhuri Morogoro, CCM Kirumba na Sheikh Amri Abeid umekamilika na sasa shughuli za kusimika mfumo huo kwenye Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam zinaendelea," amesema zaidi Mpina.
    Ameendelea kueleza kuwa mfumo huo utaongeza mapato kwa serikali kwa kiwango kikubwa, TFF, klabu na wachezaji watanufaika pia.
    Amesema mfumo huo ulileta matokeo chanya uliotumika katika maeneo kama TANAPA, KCMC na TRA (Holili, Mtukula, Sirari, Horohoro, Namanga na Tunduma) ambako CRDB imeweka mfumo huo ukisaidia kuongeza mapato kwa asilimia 200 hadi asilimia 300. 
    "TRA kabla ya kuanza kutumia mfumo huu, mapato yake yalikuwa Sh. bilioni 12 kwa mwaka lakini sasa yamepanda hadi Sh, bilioni 120 kwa mwaka baada ya kutokana na matumizi ya ETS. KCMC ilikuwa ikipata Sh. milioni mbili kwa siku lakini sasa inapata Sh. milioni 12 kwa siku na TANAPA ilikuwa ikikusanya Sh. bilioni 72 kwa mwaka (2008), lakini mapato yameongezeka hadi Sh. bilioni 121 (mwaka 2013)," amesema.
    Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu juu ya uhujumu wa mapato unaofanya na baadhi ya watendaji wa TFF kupitia njia mbalimbali ikiwamo ya kutengeneza tiketi bandia wakishirikiana na baadhi ya wadau wa soka nchini.
    Miongoni mwa viwanja vinavyodaiwa kuwa na uhujumu mkubwa wa mapato ni Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAIAGIZA TRA IISHUGHULIKIE TFF YA MALINZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top