ENGLAND imetoka sare ya 2-2 na Ecuador katika mchezo wa kujiandaa na Kombe la Dunia jana uliopigwa mjini Miami nchini Marekani jana.
Refa Jair Marrufo aliwatoa kwa kadi nyekundu, Antonio Valencia na Rahim Sterling baada ya kugombana uwanjani.
Mabao ya Ecuador yalifungwa na Enner Valencia na Michael Arroyo, wakati ya England yalifungwa na Wayne Rooney na Rickie Lambert.
Kikosi cha England kilikuwa; Foster, Milner, Shaw/Stones dk74, Jones, Smalling, Lampard, Wilshere/Lallana dk87, Oxlade-Chamberlain/Flanagan dk63, Barkley/Henderson dk84 na Rooney/Sterling dk64, Lambert/Welbeck dk84.
Ecuador: Banguera, Paredes/Achilier dk90, Guagua, Erazo, Walter Ayovi, A. Valencia, Noboa/Mendez dk50, Montero/Arroyo dk68, E. Valencia/Ibarra dk83, Gruezo/Saritama dk90 na Caicedo/Rojas dk46.
La kwanza: Enner Valencia akiifungia bao la kwanza Ecuador dhidi ya England jana



.png)
0 comments:
Post a Comment